Download App

Chapter 76: HAWEZI KUKUUMIZA

"Ulikuwa unaumwa binti yangu, mbona Ed hakusema" mama akamuuliza Lyn ambaye aliinuka na kurejea alipokuwa amekaa

"Niliugua ghafla tu tulipotoka hoteli na Ed" Lyn akajibu huku macho yake yakimwangalia Aretha ambaye bado hakuwa ameelewa chochote zaidi ya akili yake kuwaza iwapo Ed alimdanganya au la.

"Daktari anasema ni hali ya kawaida kwa mtu kuanguka kutokana na mshangao wa kitu ambacho hakukitegemea, ndio maana aliniruhusu kutoka nilipozinduka tu" Lyn akaendelea kuongea

"Ulishangazwa na nini?" Coletha akauliza kwa ukali

"Aaaah wifi si unamjua kaka yako na suprise zake" Lyn aliongea akimwangalia macho mama kama mtu mwenye kuona aibu kusema..

"Ni nini mwanangu?" Mama aliuliza huku akijaribu kutuliza akili yake baada ya kusikia Lyn akimuita bintiye 'wifi'. Bado hakuelewa kuwa Ed aliamua kuwa na Lyn au la!

"Mama aah, kabla sijazirai tulikuwa tunakuja kwako kuomba baraka za kuwa wachumba rasmi, sasa nilipatwa mshtuko sababu hakuwa ameniambia" Lyn sasa aliinama chini huku akiibia kumuangalia Coletha ambaye macho yake yalionesha kukerwa na maneno yale lakini pia alimuangalia Aretha.

Kama mshale uliolengwa mahali pasipo kukosea, Aretha aliyekuwa anamsikiliza Lyn akahisi ngazi hadi kwenye miguu. Lakini akajitahidi kutoonesha mshangao wowote

"Aaah kumbe, pole mwanangu, unaendeleaje sasa?"

Kabla ya Lyn kujibu simu yake ikaita....

"Hello Ed" akapokea

"Uko wapi?" Sauti ya Ed ilikuwa ya chini ambayo ni dhahiri alikaribia kupasuka kwa ghadhabu

"Niko nyumbani na mama, Coletha na____"

Kabla ya kumaliza simu ikakata. Lyn akamgeukia mama, "Ed atakuwa kaona hiyo taarifa Insta ngoja nimsubiri tuone tunaepushaje hizi tetesi"

Mara simu ya Aretha ikaita na kuwashtua pale sebuleni wakamwangalia, lakini yeye aliangalia kioo cha simu na hakupokea akakata kisha akazima simu.

"Mama samahani naomba kuangalia bustani ya maua kabla sijaondoka" Aretha akasema akimuangalia mama ambaye naye alimuangalia kwa macho ya huruma..

"Coletha mpeleke binti yangu bustanini, labda atanipa ushauri wa nini cha kuongeza kwenye maua yangu!"

Coletha alishukuru sana kwa wazo hilo hakutaka kukaa pale kumsikiliza tena Lyn.

"Twende dear, kule hewa yake ni nzuri kuliko ya humu ndani sasa"

Aretha akainuka akitoka na Coletha hadi mlangoni. Wakaondoka kuelekea bustanini wakimuacha Lyn na mama ndani. Wakiwa wanaenda simu ya Coletha ikaita, alipoangalia akajua kwa hali ilivyo hawezi kuongea mbele ya Aretha..

"Aretha dear endelea kuangalia, ngoja niongee na simu"

Aretha akaachia tabasamu kukubaliana na wazo la Coletha. Ukweli ni kwamba alitamani kuwa na muda wa peke yake pale bustanini kutafakari

"Hello Bro" Coletha alipokea

"Coletha, Aretha bado yuko hapo nyumbani" aliuliza Ed

"Yupo huku bustanini, bro ni nini kinaendelea maana Lyn yuko hapa mambo anayomwambia mama yanachanganya"

"Amemwambia nini?" Akauliza Ed kwa haraka

"Amemuonesha hizo habari za Insta, lakini kasema unamtambulisha hivi karibuni"

"Mmmmmm" Ed akaguna

Coletha akajua kaka yake amekaribia kumkunja mtu..

"Amesema hayo mbele ya Aretha?" Akauliza Ed

"Ndio bro, halafu Aretha ni nani hasa maana unatuchanganya h____"

Simu ikakatwa

"Ghooosh, nini kinaendelea hapa?"

Coletha akarudi alipokuwa Aretha ambaye alimkuta akiendelea kuangalia maua huku mengine akiyawekea udongo vizuri..

"Dear ungesema nikuletee glovu unachafua mikono yako"

" Aaah h.hapana usijali nitanawa mikono nikimaliza." Akajibu na kuendelea kuweka udongo

"Aretha" Coletha akamuita

"Aamhh" akaitika Aretha huku akiendelea kushindilia udongo kwenye ua mojawapo

"Usimsikilize huyo mwanamke na uongo wowote atakaosema..nakuomba" Coletha akamsihi

"Eeeh" Aretha akashtuka na kuinuka..

"Mimi sijui kuna nini kinaendelea kati yako na bro Ed, lakini nafikiri anakujali sana na hawezi kufanya kitu kukuumiza. Lyn ni muigizaji daraja la kwanza, don't fall for her lies" Coletha akamtahadharisha

"Ammhhh," Aretha akainama tena kuendelea kuweka ua vizuri huku akitifua udongo ili kupata maji kwa urahisi.

"Aretha, unadhani kaka alikuwa anajua kama Lyn yupo hapa?"

"Mmmh?"

"Alikuwa hajui ndio maana alimuuliza yuko wapi."


Load failed, please RETRY

Weekly Power Status

Rank -- Power Ranking
Stone -- Power stone

Batch unlock chapters

Table of Contents

Display Options

Background

Font

Size

Chapter comments

Write a review Reading Status: C76
Fail to post. Please try again
  • Writing Quality
  • Stability of Updates
  • Story Development
  • Character Design
  • World Background

The total score 0.0

Review posted successfully! Read more reviews
Vote with Power Stone
Rank NO.-- Power Ranking
Stone -- Power Stone
Report inappropriate content
error Tip

Report abuse

Paragraph comments

Login